Kiungo Samir Nasri ameachwa katika
kikosi cha Ufaransa kitakachocheza Kombe la Dunia, ikiwa ni siku
mbili tu kupita tangu aisadie timu yake ya Manchester City kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Mbali na Nasri, mchezaji mwenzake wa
Manchester City Gael Clichy nae ameachwa nje ya kikosi cha taifa
kinachonolewa na Didier Deschamps.
Wakati huo huo mshambulia wa Tottenham,
Erik Lamela pamoja na mshambuliaji wa Juventus Carlos Tevez nao
wamejikuta wakiachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina
itakayocheza michuano ya Kombe la Dunia.
Nao uteuzi wa kikosi cha Brazili
kitakachocheza michuano hiyo umeshuhudia kuachwa kwa wachezaji wawili
wa AC Milan wenye majina makubwa ambao ni Kaka na Robinho, wakati
Luiz Felipe Scolari akitangaza kikosi chake cha wachezaji 23, ambacho
pia kimemuacha kiungo wa PSG Lucas Moura.
Kaka na Robinho


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni