Waziri Mkuu wa zamani wa
Italia Silivio Berlusconi anatarajia kuanza kutekeleza adhabu ya
kutumikia jamii katika nyumba ya kuwahudumia wazee karibu na Jiji la
Milan.
Berlusconi alihukumiwa
miaka minne jela kwa kukwepa kodi mwaka jana, na kubadilishwa kuwa
adhabu kuwahudumia wazee waliopoteza kumbukumbu kwa muda wa saa nne
katika makazi yao.
Makazi hayo ya wazee
yanayomilikiwa na Kanisa Katoliki yamesema Berlusconi atachukuliwa
kama wanavyochukuliwa wasaidizi wa kawada katika nyumba hiyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni