Divock Origi Okoth wa kati kati
Vyama vya soka, makocha na mashabiki
wa mchezo huo nchini Kenya, wamepokea kwa hisia tofauti uamuzi wa
mchezaji Divock Origi Okoth, kuamua kuchezea timu ya taifa ya
Ubelgiji badala ya taifa lake la Kenya.
Wakati wadau wa soka wa Kenya wakiwa
katika mkanyanyiko wa mawazo, mchezaji huyo ameelezea hisia zake na
furaha aliyonayo ya kwa kupata nafasi ya kuliwakilisha taifa lake
kwenye michuano ya kombe la dunia.
Divock mwenye umri wa miaka 19, ni
mtoto wa aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Kenya Mike Origi Okoth,
ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji cha wachezaji 24,
na kuondoa nafasi ya kinda huyo kuiwakilicha nchi ya wazazi wake ya
Kenya.
Mkuu wa Utawala wa Soka Kenya Robert
Asembo amesema Kenya ilikuwa inamuhitaji Okoth kutokana na kuwa na
kipaji cha soka cha aina yake lakini kutokana na uamuzi wake huo
wanamtakia kila la kheri kama wanavyomtakia kila la kheri rais Barack
Obama.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni