WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekemea tabia ya migogoro inayojitokeza baina ya Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri kwani inaendekeza maslahi binafsi badala ya kujali maendeleo ya wananchi.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Mei 14, 2014) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 30 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kwenye ukumbi wa Naivera Complex jijini Tanga. Mkutano huo wa siku nne, ulianza jana Jumanne, Mei 12, 2014.
"Kitendo kilichotokea Manispaa ya Bukoba hakijanipendeza hata kidogo kwa sababu kitasababisha Manispaa hiyo ishindwe kutumia sh. Biliomi 17 ambazo zilitengwa kwa ajili ya kazi za maendeleo za wananchi wa mji wa Bukoba," alisema.
"Tulimuomba Meya ajiuzulu ili kuleta amani. Hii ni kwa sababu vikao vilikuwa havifanyiki kutokana na malumbano yaliyokuwepo. Yeye mwenyewe akatamka rasmi kuwa anajiuzulu, wakaleta barua rasmi nami nikawajibu kuwashukuru... baadaye madiwani wakaenda mahakamani na kufungua kesi kupinga vikao visifanyike," alifafanua.
"Kuna sh. Bilioni 17 zimetengwa kwa ajili ya kazi za maendeleo na kuboresha Manispaa ya Bukoba, lakini hizi zitarudishwa zilikotoka kwa sababu ya kujali maslahi binafsi. Wanaoteseka ni wananchi wa Bukoba wasio na kosa lolote," alisisitiza.
"Nawasihi Maweya na Wenyeviti wa Halmashauri mliopo hapa tuache ubinafsi, tuweke mbele maslahi ya wananchi. Inapotokea mtu mmoja akajiuzulu kwa ajili ya watu wengi ni baraka.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwataka Mameya na Wenyeviti hao wanasimamia tatizo la madawati na kuhakikisha linakwisha kwani nyenzo wanazo kupitia Halmashauri wanazoziongoza.
“Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa Tanzania ina mahitaji ya madawati 3,302,678 wakati madawati yaliyopo ni 1,837,783 kwa hiyo tuna upungufu wa madawati 1,464,895 katika shule zetu za msingi,” alisema Waziri Mkuu.
"Hivi Mameya mnakubali watoto wetu wakae chini kweli? Mbao mnazikamata halafu mnazinadi, kwa nini msizitumie kuchonga madawati ili kupunguza tatizo hili kwenye shule zetu?
Waziri Mkuu alisema amevutiwa na waendesha kipindi cha 'Maisha Plus' ambao wameweza kutengeneza madawati 30 katika kipindi kifupi.
"Hapa nimebaini tatizo siyo fedha bali ni dhamira. Kama 'Maisha Plus' wameweza ni kwa nini sisi tunashindwa? Alihoji.
Aliwataka viongozi hao waweke lengo la kuhimiza makazi bora kwa wananchi. "ALAT inatimiza miaka 30, wekeni azimio la kuhakikisha mnaboresha makazi ya wananchi mnaowaongoza. Wekeni utaratibu wa kujenga nyumba 20 za kisasa kila mwaka katika kila kijiji, hili linawezekana mkiamua," alisisitiza.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATANO, MEI 14, 2014

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni