Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wafanyakazi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya kulanao pamoja chakula katika fahla ya kuwapongeza wafanyakazi hao baada ya kupitishwa bajeti za Wizara hizo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea ,hafla hiyo ilifanyika leo viwanja vya Ikulu,(wapili kulia)Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abulhamid Yahya Mzee,(kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala BoraDkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (wapili kulia) wakiwapongeza wafanyakazi mbali mbali wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika hafla ya chakula iliyofanyika baada ya kupitishwa bajeti za Wizara hizo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Ikulu, Zanzibar.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni