Mshindi wa tuzo ya Oscar mwenye
asili ya Kenya Lupita Nyong'o pamoja na nyota wa filamu ya Game Of
Thrones, Gwendoline Christie ni miongoni mwa waigizaji wapya
waliopata dili la kujiunga hivi karibuni katika upigaji picha ya
filamu ya mpya ya Star Wars.
Lupita aliyetwaa tuzo hiyo kutokana
na kushiriki vyema kwenye filamu ya 12 Years A Slave ataungana na
nyota wengine kama John Boyega, Daisy Ridley, Adam Driver, Oscar
Isaac, Andy Serkis, Domhnall Gleeson, na Max von Sydow katika filamu
hiyo mpya itakayoongozwa na J.J. Abrams.
Katika kuonyesha furaha aliyonayo
Lupita ameandika kwenye Instagram yake pamoja na kuweka picha ya Logo
ya Star Wars, kuwa anaelekea kwenye galaxy mbali mbali kabisa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni