Wataalam wa afya wamesema ukosefu wa
dawa za kupunguza maumivu kwa wagonjwa wanaoelekea kufariki dunia ni
jambo linalopaswa kutafutiwa ufumbuzi wa dharura wa kiafya duniani.
Takwimu zinaonyesha watu milioni 18
wengi wao wakitokea kwenye nchi zinazoendelea walifariki dunia wakiwa
kwenye maumivu makali yasiyo ya lazima, ambapo nchini Ethiopia
mgonjwa mmoja wa saratani alijiua kwa kujirusha mbela ya lori na
kugonwa ili kuepuka maumivu.
Muungano wa Dunia wa Kuwajali
Wagonjwa waliokwenye maumivu makali umesema sehemu ya tatizo hilo la
ukosefu wa dawa za maumivu ni vitendo vya serikali kukataa kuwapatia
wagonjwa hao dawa ya kuzuia maumivu kama vile ya morphine.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni