Mmiliki wa timu ya mpira wa kikapu
ya Los Angeles Clippers Donald Sterling amekubali kuiuza timu hiyo kwa dola bilioni 2, na
kuondoa kesi aliyoufungulia uongozi wa Ligi ya Kikapu ya Marekani
(NBA).
Mwanasheria wake Maxwell Blecher,
amesema mteja wake aliyekabiliwa na tuhuma za ubaguzi wa rangi
amekubali kumaliza tafauti zote na uongozi wa NBA.
Timu hiyo sasa itanunuliwa na
aliyekuwa mtendaji mkuu wa Microsoft Steve Ballmer kwa dau hilo
litakaloweka rekodi.
Sterling alipigwa faini ya dola
milioni 2.5 na kufungiwa maisha kujihusisha na ligi ya kikapu
Marekani baada ya kutoa matamshi ya kibaguzi mbele ya umma.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni