Chama cha Ngumi nchini Kenya (BAK)
kinahitaji shilingi milioni 7 ili kuweza kuipeleka timu yote ya
mabondia 12 katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika
itakayofanyika East London nchini Afrika Kusini kuanzia Juni 14 hadi
25.
Kiongozi wa chama hicho John Kameta
amesema kutuma kikosi chote cha timu ya mabondia katika michuano hiyo
mikubwa ya Afrika kutaongeza fursa ya matarajio yao ya kupata medali
nyingi.
Kameta aliyekuwa akiongea jana huko
Mombasa amesema wamepokea mwaliko kutoka kwa wenzao wa Afrika Kusini
na tayari wameshaiarifu Wizara ya Michezo pamoja na Kamati ya Taifa
ya Olimpiki Kenya juu ya suala hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni