.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 5 Juni 2014

UINGEREZA YA BANWA NA ECUADOR HUKU ALEX OXLADE-CHAMBERLAIN AKIUMIA

Raheem Sterling alijikuta akitolewa kwa kadi nyekundu huku Alex Oxlade-Chamberlain akipata jeraha la goti wakati Uingereza ikicheza mpira usioeleweka na kujikuta ikitoka sare ya mabao 2-2 na Ecuador katika mchezo wa kujiandaa na Kombe la Dunia huko Miami, Marekani.


Mchezaji huyo kijana wa Liverpool Sterling alitolewa mnamo dakika ya 11 baada ya kugombana na mchezaji wa Manchester United Antonio Valencia ambaye naye aliambulia kadi nyekundu kwa kukasirishwa baada ya kuchezewa vibaya na Sterling, katika mchezo huo ambao Wayne Rooney na Lambert walipachika mabao.

Matokeo mengine ya mechi hizo za kirafiki za Kimataifa yalikuwa ni Uholanzi 2 - 0 Wales, Italia 1 - 1 Luxembourg, Ugiriki 0 - 0 Nigeria, Mexico 0 - 1 Bos-Herce, Gibraltar 1 - 0 Malta, Algeria 2 - 1 Romania, Hungary 1 - 0 Albania, Iceland 1 - 0 Estonia na Argentina 3 - 0 Trinidad and Tobago. 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni