Mshambuliaji wa Hispania Diego Costa
amefaulu vipimo vya afya alivyofanyiwa na timu ya Chelsea baada ya
timu hiyo kuwasilisha ombi la kumtwaa kwa paundi milioni 32 kutoka
Atletico Madrid.
Timu ya Chelsea imefanikisha dau
hilo lililokuwa limewekwa ili kumtwaa Costa kutoka Atletico na sasa
atafanya mazungumzo kuhusiana na maslahi yake binafsi.
Costa amefunga magoli 36 katika
michezo 52 aliyocheza katika msimu huu akiwa na Atletico na kuisaidia
timu hiyo kutwaa kombe la La Liga kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996
pamoja na kufikia hatua ya fainali ya Ligi ya Klabu Ulaya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni