Nchi ya Afrika Kusini inaongoza kwa
kuwa na kiwango kibaya zaidi katika ya hisabati na Sayansi, jambo
ambalo limeelezwa na kambi ya upinzani kama janga la taifa.
Chama cha Upinzani cha Democratic
Alliance kimetaka kuitishwa tathimini yakinifu ya walimu wote wa
masomo ya hisabati, Sayansi pamoja na Teknolojia.
Utafiti wa Shirika la Uchumi Duniani
(WEF) uliofanywa katika nchi 148 umeiweka Afrika Kusini katika nafasi
ya 146 kwa kufanya vibaya katika masomo hayo ikiwa chini ya Kenya,
Nigeria na Zimbabwe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni