Rais Barack Obama wa Marekani
amekutana na rais mteule wa nchi hiyo Petro Poroshenko huko Jijini
Warsaw nchini Poland na kuahidi kuisaidia kiuchumi nchi hiyo.
Rais Obama amesema atatoa msaada kwa
serikali ya nchi hiyo kulipa bili ya gesi ya kampuni ya Urusi ya
Gazprom ambayo imetishia kuikatia huduma hiyo Ukraine.
Nchi ya Ukraine imekuwa ikiyumba
kiuchumi tangu kati kati ya mwaka 2012.
Rais Obama yupo nchini Poland
kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 25 ya kumalizika kwa
ukomonisti.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni