Baadhi ya wanajeshi DRC walihukumiwa kifungo kwa kubaka mwezi Mei
Taasisi ya Uingereza imesema kuwa
maafisa usalama wamekuwa wakiwabaka mara kwa mara wanawake magerezani
katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kama adhabu ya
misimamo yao ya kisiasa.
Taasisi hiyo ya Freedom From Torture
imesema ripoti za kitabibu zilizofanywa kwa wanawake 34 zimeonyesha
wengi ya wanawake wamebakwa na makundi ya wanaume.
Wanawake hao ambao miongoni mwao ni
wafanyabiashara na wanataaluma nyingine wenye umri kati ya miaka 18
hadi 62 wanatafuta hifadhi nchini Uingereza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni