.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 2 Juni 2014

MFALME JUAN CARLOS WA HISPANIA ANG'ATUKA

 Mfalme wa Hispania Juan Carlos ( kulia ) akiwa na mtoto wake Prince Felipe pamoja na malkia Letizia. Picha hii ilipigwa mwaka 2006. 

Mfalme wa Hispania, Juan Carlos ameachia ngazi baada ya miaka 39 ya kuwa mfalme wa nchi hiyo. 

Juan Carlos aliyerithi kiti hicho cha ufalme mwaka 1975 toka kwa Francisco Franco, kuondoka kwake kunamaanisha kuwa mtoto wake Felipe mwenye miaka 45 ndiye atakuwa mfalme wa taifa hilo. 

Inasemekana hali yake ya kiafya ndiyo sababu kubwa ya kung'atuka, na hivi karibuni alifanyiwa upasuaji mara tano ndani ya miaka miwili.
Mfalme Juan Carlos na mkewe Malkia Sofia walipomtembelea Papa John Paul mwaka 2003.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni