.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 4 Juni 2014

UNAWEZA KUCHEZA KANDANDA NA SIMBA?

 UNAWEZA HII!! Kevin Richardson akisakata kandanda na simba watatu katika hifadhi ya wanyama nchini Afrika Kusini. Hii ilikuwa katika kampeni ya kampuni ya Uholanzi Van Gils ya kutangaza suti na vifaa vingine vya michezo zitakazotumika na timu ya taifa ya Uholanzi katika fainali za kombe la dunia zitakazoanza nchini Brazil kuanzia June 12 mwaka huu.
 Kevin mwenye miaka 40, anasema amekuwa akiifanya kazi ya kutunza wanyama kwa kipindi kirefu cha maisha yake, na Simba hao amewatunza tangu wadogo, kuwalisha, kuwaangalia afya zao na hata kulala nao bila matatizo yeyote.
 HAPA HUPITI!! Simba huyu akiwa tayari kumkaba na kumnyang'anya Kevini mpira katika mchezo wao wa kirafiki usiokuwa na mwamuzi.
                                                           Kevin akiwa amemkumbatia Simba dume
                       TWENDE RAFIKI!! Kevin akiongozana kwa madaha na simba huyu
 MPIRA UMEKWISHA!! Kevin akiwa ameshika mpira huku akiangaliwa na simba aliokuwa anacheza nao.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni