Waziri mpya wa Maendeleo ya Vijijini
nchini India Gopinath Munde amefariki dunia katika ajali ya gari
katika mji mkuu wa nchi hiyo Delhi.
Munde alikuwa akielekea kwenye
uwanja wa ndege kupanda ndege kurejea kwenye jimbo analoishi la
Maharashtra wakati gari alilopanda lilipogongwa na gari lingine.
Marehemu Munde alichaguliwa wiki
iliyopita kuwa Waziri wa Maendeleo ya Vijijini na serikali mpya ya
Waziri Mkuu Narendra Modi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni