Mshambuliaji wa Liverpool Luis
Suarez amewasili katika kambi ya timu ya taifa ya Uruguay hapo jana
ikiwa ni siku chache tu kupita baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye
goti lake.
Mchezaji huyo wa Ligi Kuu ya
Uingereza anamatumaini ya kuisaidia timu yake kushinda mchezo wao wa
ufunguzi wa kombe la dunia dhidi ya Costa Rica hapo Juni 14.
Na uwezekano wa yeye kushuka dimbani
umeimarisha ari katika timu ya taifa ya Uruguay na tayari daktari
wake Alberto Pan ametanabaisha kuwa mshambuliaji huo ameelekea kupona
baada ya kufanya mazoezi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni