Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard
ametangaza ataondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuitumikia katika
michezo kadhaa kwa muda wa miaka 13.
Mchezaji huyo wa Uingereza mwenye
umri wa miaka 35, anaongoza kwa kuifungia Chelsea jumla ya magoli
211, kwa sasa mkataba wake umeisha.
Tangu ajiunge na Chelsea akitokea
West Ham mwaka 2001, Lampard ameshinda makombe 11 yakiwemo matatu ya
Ligi Kuu ya Uingereza na la Kombe la Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2012.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni