Muingereza Andy Murray amemtoa
Fernando Verdasco kwa kupata ushindi wa seti zote kwenye michuano ya
tenesi ya Wazi ya Ufaransa na kutinga robo fainali ya michuano hiyo.
Bingwa huyo wa Wimbledon alipambana
kiume na kushinda seti 6-4 7-5 7-6 (7-3), na sasa atakutana na
Mfaransa Gael Monfils siku ya jumatano.
Naye Rafael Nadal ameonekana
kuimarisha mipango yake ya kutaka kutwaa kwa mara ya tano ubingwa wa
michuano hiyo kwa kutinga robo fainali kwa seti 6-1 6-2 6-1 dhidi ya
Dusan Lajovic.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni