
Mabingwa watetezi wa kombe la Dunia, Hispania wao wamefikia katika hoteli ya Master Express iliyopo Curitiba. Huu ni muonekano wa moja ya vyumba vya hoteli hiyo.

Uholanzi wenyewe wamefikia katika hoteli ya Caesar Park iliyopo katika ufukwe wa Ipanema jijini Rio de Janeiro.

Wenyeji wa michuano hii ya fainali za kombe la Dunia, Brazil wao wamefikia Atelier Molinaro Boutique Hotel.

Timu ya taifa ya Italia imefikia Portobello Resort & Safari iliyopo nje kidogo ya jiji la Mangaratiba.

Hii ni hoteli ya JP ambayo ipo katika mji wa Ribeirao Preto. Wachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya Ufaransa wamefikia katika hoteli hii.

Timu ya taifa ya Ujerumani yenyewe imefikia Toko Village

Timu ya taifa ya Ureno imefikia Royal Palm Plaza Resort iliyopo katika mji wa Campinas.

Huu ni muonekano wa moja ya vyumba vinavyopatikana Boulevard Express, ambapo timu ya taifa ya Argentina wamefikia.

Timu ya taifa ya Ubelgiji wamefikia Paradise Golf & Lake Resort.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni