.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 28 Julai 2014

BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LATAKA KUSITISHWA MAPIGANO GAZA BILA YA MASHARTI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetaka kuitikiwa mara moja wito wa kusitisha mapigano bila vikwazo vyovyote katika ukanda wa Gaza.


Mkutano wa dharura wa baraza hilo umeunga mkono wito wa kusitisha mapigano kufuatia Sikukuu ya Idd El Fitri na hata baada ya siku kuu hiyo.

Hapo jana Israeli na Wapiganaji wa Palestinia hapo jana wameendelea na mapigano licha ya kauli ya kusitisha mapigano kwa saa 24 uliotangazwa na Hamas.

Zaidi ya Wapalestina 1,030 wengi wao wakiwa ni raia wamekufa, ambapo pia wanajeshi 43 wa Isareli wameuwawa pamoja na raia wawili.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni