Alhamisi, 31 Julai 2014
BARAZA LA WAWAKILISHI MAREKANI LATAKA KUMFUNGULIA MASHTAKA RAIS OBAMA
Baraza la Wawakilishi la Marekani limepitisha azimio la kumshtaki Rais Barack Obama kwa madai ya kuenda kinyume na mamlaka yake ya Kikatiba.
Kura 225 dhidi ya 201 zilizopigwa kwa misingi ya kisiasa zinatoa fursa kwa mawakili wa baraza hilo kuandaa nakala za kisheria kwa ajili ya kufungua kesi hiyo.
Wanaounga mkono azimio hilo wanasema Rais Obama alivuka madaraka yake wakati alipochelewesha muda wa kikomo wa bima katika mpango wa sheria ya afya.
Hata hivyo Rais Obama amepuuzia mpango huo wa kumshtaki kwa kusema ni upotevu wa muda, na kuongeza kuwa kila mtu anaonajuhudi hizo ni za kutafuta umaarufu wa kisiasa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni