TIMU ya Coastal Union ya Tanga
"Wagosi wa Kaya" kesho inatarajiwa kucheza mechi ya
kirafiki na African Sports “Wanakimanumanu”kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani itakayokuwa ya kusheherekea sikukuu ya iddi Pili.
Akizungumza leo Ofisa Habari wa
Coastal Union,Oscar Assenga amesema maandalizi ya kuelekea mchezo
huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kinachosubiriwa na mechi hiyo
itakayoanza saa kumi jioni kwenye uwanja huo.
El Siagi amesema baada ya kumaliza
mechi hiyo timu hiyo itaelekeza mipango yake ya kucheza mechi za
kirafiki nyengine ili kuweza kujiweka imara kwa ajili ya maandalizi
ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Amesema wachezaji wa timu hiyo
wataingia kwenye mechi hiyo kwa malengo ya kupata ushindi ili kuweza
kuendeleza rekodi ya kuwafunga wanakumanumanu hao ambao msimu ujao
watashiriki michuano ya ligi daraja la kwanza.
Kwa upande wake,Ofisa Habari wa timu
ya African Sports,Wanakimanumanu”Said Karsandas amesema kuwa
wamepania kushinda kwenye mechi hiyo ili kuweza kurudisha ile heshima
ya timu hiyo kwa wagosi hao wa kaya.
“Tunajua mechi hii itakuwa ni
ngumu kutokana na uwezo wa Coastal Union hivyo nasi tumejipanga
kuweza kufanya vizuri ili kutoa burudani kabambe “Alisema
Karsandas.
Hata hivyo aliwataka wakazi wa mkoa
wa Tanga na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani
itakayokuwa ikitolewa kwenye mechi hiyo .
Oscar Assenga .
Msemaji wa Coastal Union.
0714453839,Tanga.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni