Na: Shushu Joel
Wana kijiji wa kijiji cha jijabirishi
wilayani maswa mkoani simiyu wamelikamata gari aina ya center lenye
namba za usajili T 591 AFJ mali ya BASEMA lenye makazi yake jijini
mwanza.
Gari hilo lilikamatwa majira ya saa
moja jioni likiwa na nguzo za umeme 16 katika maeneo ya nyambiti
mpakani mwa wilaya ya magu na maswa zikiwa zinapelekwa mkoani mwanza
kwa ajili ya biashara.
Nguzo hizo ni mali ya kampuni ya
Sengerema Engineening Group Limited inayosambaza umeme katika vijiji
mbalimbali mkoani simiyu kwa kupitia mradi wa umeme vijijini ambao
unasimamiwa na serikali ya Jamhuli ya Muungano wa Tanzania.
Dereva wa gari hilo alinusurika kifo
toka kwa wananchi hao kwa msaada wa polisi wa kituo kidogo cha
nyambiti ambao waliwahi kufika katika tukio hilo na kuwaomba wananchi
wasifanye chochote kwani huyu dereva alikuwa ajui kinachoendelea juu
ya tukio hili kwa sababu yeye kaagizwa na boss wake ambaye ni Bw,
BASEMA kuja kuchukua mzigo huo wa nguzo za umeme.
Akizungumza mara baada ya kuokolewa na
polisi dereva wa gari hili aliyejitambulisha kwa jina la Daniel Peter
mwenye umri wa miaka 29 amesema kuwa yeye ufanya shughuli za ubebaji
wa mizigo mbalimbali na gari lake hivyo alipigiwa simu na boss na
kisha kuambiwa aweke mafuta ya laki moja kwani kuna safari ya
kilometa nyingi kidogo na kisha kufanya kama alivyoagizwa na boss
wake na ndipo alipoongozana na wenyeji wake wenye gari aina ya
....... Lenye namba za usajili T.........ambalo lilikimbia mara baada
ya timbili hilo la wananchi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
msimamizi wa mradi huu wa umeme vijiji toka katika kampuni ya
sengerema Engineening Group limited Bw, Juma musime amesema kuwa
wakiwa katika kazi zao za usambazaji wa nyaya toka sehemu moja kwenda
sehemu nyingine mara
anapigiwa simu na mwanakijiji wa
jijabirishi na kumuuliza kuwa mbona hizi nguzo zinapelekwa mwanza au
zimebaki? Ndipo hapo msimamizi huyo alipoomba msaada wake kwa
kuwataarifu wanakijiji wenzake na kuanza kuzifuatilia nguzo hizo na
kufanikiwa kuzikamata.
Bw, Juma aliongeza kuwa ukaribu wake na
wananchi hao ndio nguzo ya mafanikio ya umeme katika mkoa huo na pia
kulipongeza jeshi la polisi kwa msaada wao wa dhati na hata kuahidi
kushilikiana nao katika mambo mbalimbali yenye tija katika taifa
langu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
kamanda wa polisi mkoa wa simiyu, kamanda Charles Mkumbo amesema kuwa
ni kweli tukio hilo limetokea na mpaka sasa dereva wa gari hilo
anashikiliwa na polisi
kwa uchunguzi wa kisheria na mda si
mrefu kesi hiyo itapandishwa mahakamani.
Kamanda mkumbo aliongeza kuwa
anasikitishwa sana na watu wa aina hii kwani hawa ni wapinga
maendeleo ya taifa kabisa lakini sheria itachukua mkondo wake na hata
kuwa fundisho kwa watu wa namna hii.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni