.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 22 Julai 2014

JESHI LA POLISI NCHINI LAWAKAMATA WATU WALIOHUSIKA NA MABOMU JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini,(DCI), Isaya Mungulu, akijadiliana na maafisa wa polisi.

WATU sita wametiwa mbaroni na jeshi la Polisi Mkoani Arusha, wawili
kati yao wamekutwa na mabomu saba ya kurushwa kwa mkono, ambayo sita
kati ya hayo, yametengenezwa Urusi na moja Ujerumani.


Akizungumza leo Jijini Arusha na waandishi wa habari kwenye ofisi za
Jeshi hilo, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini,(DCI), Isaya Mungulu,
amesema mabomu hayo yamekamatwa Julai 21 mwaka huu, saa 2.00 usiku,
huko eneo la Sombetini, Manispaa ya Arusha.

Amewataja waliokamatwa kuwa ni watuhumiwa 25 ila baadhi yao ni Jafari
Lema (38) ambaye alikuwa Imamu wa Msikiti wa Masjid Quba, uliopo makao
mapya Arusha,Shabani Musa Mlinzi wa Mgahawa wa Chinese,Mohamed Nuru,
Abdul Mohamedy (31), Said Temba (31) ambaye ni mfanyabiashara wa
mabasi makubwa ya Khandahar na Athumani Hussein .

Wengine ni Yusuph Ally na mke wake Sumaiya Juma (19), ambao walikutwa
na mabomu nyumbani kwao, risasi sita za Short gurn, mapanga mawili na
bisibisi moja.


Mungulu amesema watuhumiwa hao sita wanahusika katika tukio la Julai 7
mwaka huu, katika mgahawa wa Vama Traditional uliopo eneo la uzunguni
karibu na Mahakama kuu na nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa Arusha.
Amesema kuwa wakati wowote watuhumiw ahao watafikishwa Mahakamani ili
kujibu mashitaka ya ulipuaji mabomu unaowakabili.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni