.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 21 Julai 2014

JK AFUNGUA KITUO CHA AFYA NA KUKAGUA KILIMO CHA KAHAWA MBINGA, AFUNGUA SOKO LA KIMATAIFA MKENDA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi kituo cha afya katika Gereza la Kitai wilayani Mbinga jana.Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo Alexander Richard Nyefwe. Kituo hicho kitatoa huduma kwa askari magereza,wafungwa na vijiji jirani.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miche bora ya kahawa mkulima mdogo Bi Dorothea Komba wakati alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam katika kijiji cha Lipokela wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma leo.Kampuni ya Olam imepanga kutoa jumla ya miche milioni tatu kwa wakulima wadogo elfu mbili katika vijiji vinne vinavyozunguka shamba hilo katika kipindi cha miaka mitano ili kuwashirikisha kuzalisha kahawa bora.
Meneja wa Shamba la Kahawa la AVIV Farm linalomilikiwa na kampuni ya Olam Bwana Medappa Ganapati akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mche bora wa kahawa iliyozaa vyema wakati Rais alipolitembelea na kukagua shamba la kahawa katika kijiji cha Lipokela, wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.kulia ni mbunge wa Peramiho Mh.Jenister Mhagama.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma.

Sehemu ya Soko la Kimataifa la Mkenda lililopo katika kijji cha Mkenda Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania leo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma. (Picha zote na Freddy Maro).

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni