.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 28 Julai 2014

KIWANDA CHA NGUO CHA SUNFLAG JIJINI ARUSHA CHAPIGWA FAINI YA MILIONI 80 KWA KUHARIBU MAZINGIRA


WAZIRI WA MAZINGIRA MH DR BILITH MAHENGE AKIWA KATIKA ZIARA NA WAJUMBE WA NEMC KUKAGUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA NGUO CHA SUNFLAG KILICHOPO JIJINI ARUSHA.

UKAGUZI UKIENDELEA KATIKA KIWANDA CHA NGUO CHA SUNFLAG JIJINI ARUSHA
PICHA YA SHEHENA YA MAGOGO YALIYOKUTWA KIWANDANI HAPO YAKISUBIRI KUTUMIKA KATIKA UZALISHAJI.
VIONGOZI WA KIWANDA CHA NGUO CHA SUNFLAG WAKITOA MAELEZO KWA WAZIRI WA MAZINGIRA, MH MAHENGE 

BARAZA LA UHIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA (NEMC) LIMEKITAKA KIWANDA CHA KUTENGENEZA NGUO CHA SUNFLAG KILICHOKO JIJINI ARUSHA KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 80 NA KUPANDA MITI ZAIDI YA ELFU SABA (7.000) KAMA FIDIA BAADA YA KUKUTWA NA SHEHENA KUBWA YA MAGOGO NA MITI YA ASILI AMBAYO NI UHARIBIFU MKUBWA WA MAZINGIRA

HATUA HIYO IMEKUJA BAADA YA WAZIRI WA MAZINGIRAA NA WATENDAJI WA BARAZARA HILO KUTEMBELEA KIWANDA HICHO NA KUKUTA SHERIA MBALIMBALI ZIKIWA ZIMEKIUKWA IKIWEMO YA KUKATA NA KUTUMIA MITI YA ASILI KAMA NISHATI JAMBO AMBALO NI UKIUKWAJI WA SHERIA ZA MAZINGIRA

AKIZUNGUMZIA HALI HIYO WAZIRI WA MAZINGIRA MH DR BILITH MAHENGE AMESEMA KAMA KIWANDA HICHO HAKITAWEZA KUBADILISHA MFUMO WA KUTUMIA KUNI KAMA NISHATI HADI MWEZI WA KUMU MWAKA HUU KITALAZIMIKA KUFUNGWA KWANI HAIWEZEKANI KUENDELEA NA MATUMIZI YA KUNI

MENEJA MWENDESHAJI WA KIWANDA HICHO BW HARUN MAHUNDI PAMOJA NA KUKIRI KUWEPO KWA CHANGAMOTO YA NISHATI AMESEMA WAO HAWASTAHILI KUBEBA TUHUMA ZA KUHARIBU MAZINGIRA KWANI WANANUNUA MAGOGO NA MITI AMBAYO TAYARI IMESHAKATWA TENA KWA NJIA ZILIZO HALALI



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni