.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Julai 2014

MAPIGANO KATI ISRAEL NA HAMAS YASITISHA SAFARI ZOTE ZA MASHIRIKA YA NDEGE YA ULAYA KUELEKEA TEL AVIV

 Mashiriki mengi ya ndege barani Ulaya yamesitisha safari zake kuelekea nchini Israel kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya taifa hilo na kundi la Hamas lililopo katika ukanda wa Gaza. 

Shirika la ndege la Delta, Shirika la ndege la Marekani na mashirika mengine ya ndege ya Ulaya yametangaza kusimamisha safari zake zote kuelekea katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion ulipo mjini Tel Aviv. 

Hapo jana jumanne ndege ya Delta namba 468 Boeing 747 iliyokuwa inatoka New York kuelekea Tel Aviv ikiwa na abiria 273 na wahudumu 17 wa ndege ililazimika kukatisha ruti hiyo na kuelekea Paris, Ufaransa kufuatia taarifa kuwa hali si shwari mjini Tel Aviv.
Taarifa za mashirika hayo kusitisha safari zake zimekuja baada ya kuripotiwa kuwa, makombora ya Hamas yameshambulia na kuharibu nyumba moja jirani na uwanja huo wa ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni