Marekani imeendelea kuiwekea vikwazo zaidi Urusi, hii ni kufuatia mgogoro unaoendelea nchini Ukraine ambapo Urusi inawaungwa mkono waasi wanaoipinga serikali iliyopo madarakani.
Akihutubia usiku wa kuamkia leo akiwa ikulu ya Marekani White House, Rais Barack Obama amesema kuwa vikwazo hivyo ni katika sekta za Nishati, Silaha na Fedha.
Katika hotuba yake hiyo, Obama amesema vikwazo hivyo kwa Urusi haviwezi kuanzisha vita baridi.
Aidha ameitaka Urusi kuacha kuwaunga mkono waasi na kuyaondoa majeshi yake katika mpaka wa Ukraine, huku pia akisisitiza Urusi ifanye juhudi za kuhakikisha waasi wanarejea katika meza ya mazungumzo ili kumaliza machafuko.
Rais wa Urusi, Vladmir Putin


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni