.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 25 Julai 2014

MIILI ZAIDI YA ABIRIA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE YA MALAYSIA MH17 YAWASILI UHOLANZI

 Miili mingine 74 kati ya 298 ya abiria waliopoteza maisha katika ajali ya ndege ya Malaysia iliyotunguliwa na waasi nchini Ukraine  imewasili nchini Uholanzi. 

Miili hiyo ambayo imesafirishwa kwa ndege maalum za kijeshi, inafanya idadi ya miili 114 kuwa imewasili nchini Uholanzi, baada ya miili mingine 40 kuwasili juzi na yote imehifadhiwa katika kambi ya kijeshi ya Korporaal van Oudheusden kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi. 

Waasi wanaoipinga serikali ya Ukraine ambao wanaungwa mkono na Urusi,waliitungua kimakosa ndege ya shirika la ndege ya Malaysia iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam, Uholanzi kuelekea Kuala Lumpur ikiwa na abiria 283 na wahudumu wa ndege 15, ambapo karibu nusu ya abiria hao ni rai wa Uholanzi na wote waliokuwa katika ndege hiyo MH17 walifariki dunia.
 Msafara wa magari maalum iliyobeba miili ya abiria 74 kutoka uwanja wa ndege mjini Eindhoven, Uholanzi kuelekea katika kambi ya kijeshi ambapo miili hiyo imehifadhiwa kwa kufanyiwa uchunguzi maalum. 



Hakuna maoni :

Chapisha Maoni