.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 28 Julai 2014

MKENYA NDIKU ATWAA MEDALI YA DHAHABU KATIKA MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA

Mkenya Caleb Mwangangi Ndiku ametwaa medali ya dhahabu katika michuano ya Jumuiya ya Madola katika mbio za mita 5,000, na kulifanya taifa lake kupata medali ya dhahabu ya pili katika michuano hiyo.

Hata hivyo katika mbio hizo shujaa alikuwa kijana wa miaka 17 kutoka kisiwa cha Solomon Rosefelo Siosi ambaye alimaliza mbio hizo wa mwisho ikiwa ni dakika tisini kupita baada ya wenzake kumaliza mbio hizo.

Siosi hakukakata tamaa aliendelea kukimbia mbio hizo huku akishangiliwa na watu hata baada ya wanariadha 23 kumaliza mbio hizo, na kufanikiwa kuweka rekodi ya taifa lake na kupata umaarufu wa ghafla katika michuano hiyo.
                                         Rosefelo Siosi akimaliza mbio hizo wa mwisho

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni