.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 28 Julai 2014

BALOZI SEIF AWAANDALIA FUTARI WANANCHI WA KIJIJI CHA NUNGWI NA WILAYA YA KASKAZINI A


Baadhi ya waumini na Wananchi wa Kijiji cha Nungwi pamoja na Wilaya ya Kaskazini “ A “ wakifutari pamoja futari iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Kituo cha Afya Nungwi.

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “ B “ Nd. Khamis Jabir Makame kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pembe Juma Khamis na Wananchi wa Mkoa huo akitoa shukrani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif baada ya kuwaandali Futari ya pamoja.
Kushoto ya Nd. Khamis Jabir ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Seif na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja Nd. Haji Juma Haji.

Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na baadhi ya wazee wa Kijiji cha Nungwi mara baada ya kufutari nao pamoja mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji na kumpa pole Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Al Hajj Mwangi Rajab Kundya baada ya kufiwa na Baba yake Mzazi.

Mzee Rajab Kundya amefariki dunia jana nyumbani kwa mwanawe Katibu huyo wa CCM Mkoa Mjini hapo Kianga Wilaya ya Magharibi na mwili wake kusafirishwa kwa Boti kupelekwa Dar es salaam kwa hatua ya mazishi.

                                                                 Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Waumini wa Dini ya Kiislamu pamoja na wananchi hapa Nchini wako katika maandalizi ya mwisho ya kusherehekea siku Kuu ya Iddi el Fitri baada ya kumalizika kwa ibada ya funga ya mwezi mtukufu wa ramadhani.

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni miongoni mwa nguzo tato za Kiislamu zinazomuwajibikia Muumini wa Dini hiyo kuzitekeleza ikitanguliwa na Kuamini uwepo wa Muungu Mmoja na Mtume Muhammad { SAW } ni Mjumbe wake, kusimamisha sala tano kwa siku, na zile mbili za mwisho za kutoa zaka pamoja na Kwenda kuhiji Maka kwa muumini mwenye uwezo.

Ibada ya funga inafikia ukingoni kwa waumini wa dini hiyo wakikamilisha kufutari pamoja katika maeneo na vitongoji tofauti kama ilivyotokea kwa Wananchi wa Kijiji cha Nungwi pamoja na wengine wa Wilaya ya Kaskazini “A”, Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Futari hiyo iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yeye binafsi na wakeze wote wawili walishiriki kikamilifu kwenye futari hiyo ilifanyika katika eneo la Kituo cha Afya cha Kijiji cha Nungwi.

Akitoa shukrani kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na wananchi wa Mkoa huo Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “ B” Nd. Khamis Jabir Makame alisema futari ya pamoja kwa waumini wa dini ya Kiislamu ni kitendo kilichoamrishwa na Mwenyezi Muungu.

Nd. Jabir alisema mfumo huo unaowakutanisha watu wa rika na jinsia tofauti hutoa fursa kwa watu hao mkubadilishana mawazo, kupeana nasafa, ushauri na hata kuonyana kwa yale mambo yanayokatazwa ndani ya vitabu vya Dini na maamrisho ya Muumba.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kaskazini “ B” alifahamisha kwamba maamrisho ya Dini yamekuwa yakihimiza kwa waumini wenye uwezo kuwajibika ipasavyo katika kuwafutarisha waumini wenzao waliowazunguuka.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni