.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 27 Julai 2014

MWANAMKE MWENYE EBOLA ALIYETOROKA HOSPITALI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJISALIMISHA

Mwanamke mmoja aitwae Saudatu Koroma raia wa Sierra Leone aliyetoroka hospitali baada ya kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola, amefariki dunia baada ya kujisalimisha tena hospitali.

Familia ya mwanamke huyo ilimlazimisha kutoka hospitali ya umma siku ya Alhamis, akiwa ni mgonjwa wa kwanza kuripotiwa katika Jiji la Freetown, ambako hakuna chumba maalum kwa wagonjwa wa Ebola.

Tangu mwezi Februari mwaka huu zaidi ya watu 660 wamekufa kwa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi, ikiwa ni mlipuko hatari kuliko wote wa ugonjwa huo kutokea duniani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni