Real Madrid imemtambulisha mchezaji
wao waliomnunua kwa paundi milioni 60, James Rodriguez baada ya
kukamilisha uhamisho na nyota huyo aliofanya miujiza katika Kombe la
Dunia anayechezea Monaco.
Nyota huyo wa Kimataifa wa Colombia
amekubali mkataba wa miaka sita na Madrid na amefanyiwa vipimo vya
afya hao jana asubuhi na baadae kuonyeshwa kwa kundi la mashabiki
katika dimba la Santiago Bernabau.
Rais wa Klabu ya Real Madrid,
Florentino Perez alimkaribisha mshambuliaji huyo na kumlinganisha na
mkongwe wa enzi hizo Alfredo Di Stefano ambaye naye alijiunga na
Madrid akitokea Colombia.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni