Msafara wa watu 25 wa kikosi cha
timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys)
unaondoka kesho (Julai 28 mwaka huu) kwenda Afrika Kusini kwa ajili
ya mechi dhidi ya Afrika Kusini (Amajimbos).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya
pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa
Dobsonville uliopo Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9 kamili mchana
kwa saa za Afrika Kusini.
Timu hizo zilitoka suluhu katika
mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam
Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam. Mshindi atacheza raundi ya
mwisho ya michuano hiyo ya Afrika na mshindi wa mechi kati ya Misri
na Congo Brazzaville.
Fainali za Afrika kwa vijana wenye
umri chini ya miaka 17 zitafanyika mwakani nchini Niger.
Wachezaji wanaounda kikosi cha
Serengeti Boys katika msafara huo utakaoondoka saa 2 usiku kwa ndege
ya Fastjet ni Abdallah Jumanne Shimba, Abdulrasul Tahil Bitebo,
Abutwalibu Hamidu Msheri, Adolf Mtsigwa Bitegeko, Ally Aziz Mnasi,
Ally Shaban Mabuyu na Athanas Enemias Mdamu.
Wengine ni Badru Haji Othman, Baraka
Yusuph Baraka, Issa Backy Athuman, Juma Ally Yusuph, Kelvin Longnus
Faru, Martin Kiggi Luseke, Metacha Boniface Mnata, Mohamed Mussa
Abdallah, Omary Ame Omary, Omary Natalis Wayne, Prospal Alloyce
Mushin na Seif Said Seif.
Benchi la Ufundi linaongozwa na
Kocha Mkuu Hababuu Ally Omary akisaidiwa na Stewart John Hall
(Mshauri wa Ufundi), Peter Manyika (Kocha wa makipa), Richard Yomba
(Daktari), na Edward Venance (Mtunza vifaa).
Msafara wa timu hiyo itakayorejea
nyumbani Agosti 4 mwaka huu unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Khalid
Mohamed Abdallah.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU
TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni