Wafanyakazi wa Nakumatt Mlimani
wakifurahia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mall hiyo Mlimani City
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt
Holdings, Atul Shah akimuonesha baadhi ya bidhaa Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe Janet Mbene wakati wa ufunguzi huo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Mhe Janet Mbene akiangalia bidhaa wakati wa ufunguzi.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Nakumatt Holdings,
imezindua rasmi tawi la kwanza kati ya matawi yake matatu makubwa
nchini Tanzania ambayo awali yalimilikiwa na Kampuni ya Shoprite ya
Afrika ya Kusini.
Ikiwa ni mpango wake mpya wa
kuboresha zaidi huduma zake, Nakumatt holdings, imezindua tawi hilo
kubwa ambalo litakuwa utambulisho muhimu wa huduma zake katika eneo
la biashara la Mlimani City litakaloitwa Nakumatt Mlimani.
Tawi hilo la 48 la Nakumatt
limepambwa kwa rangi na mwonekano wa alama za Nakumatt na kwa ubunifu
wa hali ya juu.
Pamoja na Nakumatt Mlimani, kampuni
hiyo pia iko mbioni kuzindua tawi lengine kubwa litakalojulikana kama
‘Nakumatt Pugu Road’ jijini Dar es salaam ambako pia kutakuwa
makao yake makuu. Pia itafungua Nakumatt Arusha siku zijazo.
Kwa kufungua matawi yake matatu
moja baada ya jingine, Nakumatt pia itakuwa imefikisha matawi 50
katika mtandao wake wa huduma za uuzaji bidhaa na hivyo kutekeleza
mkakati wake wa maendeleo ambao ulizinduliwa mwaka 2011.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa
duka lake la kwanza in Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Nakumatt
Holdings, Atul Shah alisema kufunguliwa kwa matawi matatu mapya
yaliogharimu takriban dola za Marekani milioni 3 ni sehemu ya mpango
wa upanuzi wa huduma za uuzaji bidhaa katika kanda ya Afrika.
Kutokana na uzinduzi wa Tawi la
Nakumatt Mlimani, Shah alisema kuwa Nakumatt sasa ina maduka mawili
makubwa yanayofanya kazi nchini Tanzania.
Nakumatt Mlimani inaungana na duka
jingine la la Nakumatt Moshi lililofunguliwa mwaka 2011 katika mji
huo ambako kuna Mlima Kilimajaro.
”Uzinduzi wa Nakumatt Mlimani ni
ndoto ya muda mrefu ambayo sasa imekuwa kweli ambapo tumekuwa
tukifikira mahali pa kuweka duka letu jijini Dar es salaam na maeneo
mengine nchini Tanzania,” alisema Shah na kuongeza:
“Uzinduzi huu pia ni hatua nzuri
itakayopelekea uzinduzi mwingine wa duka letu la 50 katikati ya
Agosti ambapo tutakuwa tumefanikiwa kufikia malengo yetu
tuliyojiwekea kuyafikia Februari mwakani.”
Maduka matatu ya Shoprite yalifungwa
mwezi uliopita ili kufanikisha kazi ya kuyaboresha zaidi sambamba kwa
kuzingatia viwango na uzoefu wa Nakumatt.
Pia Nakumatt inatarajia kufungua
matawi mengine matatu ya biashara nchini Kenya kabla ya mwisho wa
mwaka huu.
Pia kampuni hiyo itakuwa na duka
kubwa katika eneo kubwa la kifahari la Green Square mjini Kericho
nchini Kenya.
Shah alisema Nakumatt ina mkakati wa
kukuza biashara wa kampuni ambao unategemea zaidi uwepo wa vitega
uchumi ambapo kampuni inaweza kuendesha shughuli zake za maduka ya
supermaketi.
Shah aliongeza kwa kusema:
“ Kwa sasa tunaendesha shughuli
zetu katika nchi 12 na tunashirikiana na wamiliki wa maeneo ya
biashara nchini Kenya ambao wanaweza kutoa huduma za kujenga maeneo
ya maduka makubwa katika maeneo ya Machakos, Nyeri, Kajiado, Garissa,
Embu, Naivasha,Narok Busia and Homabay.”
Ili kutimiza masharti ya Nakumatt,
Shah aliwahimiza waendelezaji wa maeneo ya biashara na Mameneja wa
Miradi kushauriana na wataalam wa Nakumatt kuhusu namna ya kuboresha
uchoraji wa ramani na ujenzi wenye mvuto kwa wateja katika maduka ya
kampuni hiyo.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni