Kenya imepata medali yake ya dhahabu
ya kwanza katika michuano ya Jumuiaya ya Madola baada ya Flomena
Daniel kumuongoza mwenzake Caroline Kilel kumaliza mbio za marathoni
wanawake huku Kenya ikishika nafasi ya kwanza na ya pili hii leo.
Flomena ambaye ni mshindi wa mbio za
marathoni za Paris amemaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa saa 2
dakika 26 na sekunde 45, huku Kilel.
Muastralia Jess Trengrove alichuana
vikali na kuchukua nafasi ya tatu, na kumshinda kasi Mnamibia Helalia
Johannes.na kutwa medali ya shaba.
Katika mbio za wanaume Muaustralia
Michael Shelley aliwashangaza wengi kwa kuongoza mbio za kilomita 8,
ambazo huwa zinatwaliwa na wakimbiaji wa Afrika na kufanikiwa kutwaa
medali ya dhahabu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni