.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Julai 2014

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA

 Musa Mbeo mwenye miaka 24 ambaye ni Mnyamwezi na mkazi wa Mihogoni katika manispaa ya Tabora ambaye alikamwatwa akijifanya ni ofisa wa polisi.
 Kitambulisho cha bandia alichokuwa nakitumia kutapeli watu kwa kujifanya ofisa wa polisi.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 23/07/2014.

Ndugu waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linaendelea na operesheni ya kupambana na wahalifu na wahalifu katika operesheni hiyo tumefanikiwa kama ifuatavyo:-

KUJIFANYA ASKARI POLISI: Huko eneo la Mihogoni kata ya Mbugani manispaa ya Tabora alikamatwa Mussa S/0 Mbeo 24yrs, mnyamwezi mkazi wa mbugani akijifanya ni askari Polisi, baada ya kupekuliwa alikutwa akiwa na kitambulisho feki kilichokuwa na majina ya MOSES R.KYOMO ID NO. F8452 D/C chenye picha yake. baada ya kuhojiwa mtuhumiwa amekiri kutumia kitambulisha hicho kwa kutapeli wananchi. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara moja.

KUPATIKANA NA SILAHA TATU AINA YA GOBORE. Katika kijiji cha Kitunda kata ya Kipili wilaya ya Sikonge mkoa wa Tabora askari wakiwa doria waliwakamata watuhumiwa watatu ambao ni:-

1. PETER S/O PAULO, 48yrs, Mgogo, Mkulima, Mkazi Kipili Sikonge.

2. SULEMAN S/O IDDY, 19yrs, Mhaya Mkulima, Mkazi wa Kapumpa Sikonge.

3. JUMA S/O SUDY, 46yrs, Mnyamwezi, Mkulima, Mkazi wa Kiwele Sikonge.

wakiwa wanamiliki silaha aina ya gobore bila kibali. Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.




KUKAMATWA WATUHUMIWA WA 4 NA POMBE YA MOSHI LITA 295:- Huko wilaya kaliua na Igunga askari wakiwa doria waliwakamata watuhumiwa wanne wakiwa na pombe ya moshi lita 295 watuhumiwa hao ni:-

1. JOSEPH S/O SEBASTIAN, 48YRS, MSUKUMA MKAZI WA UYUMBU.

2. MWAJUMA d/o RAMADHAN, 40YRS, MNYIRAMBA, MKRISTO, MKULIMA WA IPUMBULIYA.

3. ROZALIA d/o SHIJA, 35YRS, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA NKINGA.

4. ASHA d/o MARCO, 27YRS, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA SIMBO.

Baada ya mahojiano watuhumiwa wamekiri kuwa ni wauzaji wa pombe hiyo. Watuhumiwa wamefikishwa mahakamani.

KUPATIKANA NA DAWA ZIDHANIWAYO ZA KULEVYA NA VIFAA VYA KUJIDUNGIA: - Huko maeneo ya Chemchem na Isevya Manispaa ya Tabora waliwakamata watuhumiwa 12 wakiwa wamejifungia ndani ya Guest House ijulikanayo kwa jina la KENIOS baada ya kupekuliwa walikutwa na sindano,nyembe na gram mbili ya madawa yadhaniwayo ni heroin watuhumiwa hao ni :-

1. HAMISI S/O HATHUMANI@ MBAO, 39YRS, M/MWEZI, MUISLAM, MKAZI WA CHEMCHEM.

2. ISSA S/O ABDALAH 22YRS MHEHE MKAZI WA CHEMCHEM

3. ALLY S/O BAKARI 34YRS MYAO MKAZI WA NG’AMBO.

4. DENSI S/O PETRO 34YRS MPOGORO MKAZI WA ISEVYA.

5. MRISHO S/O SHABANI 22YRS MNYAMWEZI MKAZI WA CHEMCHEM.

6. RAMADHANI S/O MBADE 40YRS MNYAMWEZI MKAZI WA ISEVYA.

7. HAJI S/O ABDALAH @ MUKI 40YRS MNYAMWEZI MKAZI WA ISEVYA.

8. SAID S/O KASUMARI 24YRS MUHA MKAZI WA KIGOMA UJIJI.

9. SHABANI S/O HARUNA 25YRS MUHA MKAZI WA KIGOMA UJIJI.

10. DAVID S/O MALLE 43YRS MCHAGA MKAZI WA ISEVYA.

11. RAMADHANI S/O HAMISI

12. PASCAL S/O ROBERT

watuhumiwa wakiwa wanapelekwa kituo cha polisi waliwashawishi askari kuwapa rushwa ya Tshs 90,000/= ili waachiliwe wasifikishwe kituoni. Baada ya mahojiano watuhumiwa wamekiri kuwa ni watumiaji wa madawa hayo. Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani muda wowote.

Jeshi la Polisi linazidi kutoa wito kwa wananchi kuzidi kushirikiana nalo na kutoa taarifa za uhalifu na waalifu ili kupunguza kabisa uhalifu mkoani kwetu. Pia watumiaji wa pombe ya moshi na madawa ya kulevya kuacha mara moja jeshi la polisi halitafumbia macho vitendo vyote vya kihalifu.

Imetolewa na:-

Suzan S. Kaganda –ACP.
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA TABORA.




Hakuna maoni :

Chapisha Maoni