.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 29 Julai 2014

UGONJWA WA EBOLA WASABABISHA MIPAKA YA LIBERIA KUFUNGWA

Mipaka yote inayoingia Liberia imefungwa na jamii iliyokumbwa na ugonjwa wa Ebola wanakabiliwa na zuio la kutotoka maeneo yao katika kujaribu kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo.

Vituo vya vya kupima ugonjwa huo vimewekwa katika maeneo makuu machache yanayoruhusiwa kuingia, kama vile uwanja wa ndege.

Wakati huo huo shirika kubwa la ndege la Nigeria la Arik Air, limesitisha usafiri wa ndege zake kwenda Liberia na Sierra Leone baada ya mtu aliyeugua Ebola kuingia kwa ndege Nigeria wiki iliyopita.

Ugonjwa wa Ebola umeuwa watu 660 katika nchi za Afrika ya Magharibi tangu Februari.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni