.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 6 Agosti 2014

ABIRIA MMOJA AKAMATWA BAADA YA KUTOA TAARIFA YA TISHIO LA BOMU NDANI YA NDEGE YA QATAR

 Ndege ya shirika la ndege la Qatar ikiwa inasindikizwa na moja ya ndege za kivita ya jeshi la Uingereza ( juu ) kuelekea uwanja wa ndege wa Manchester. 

Abiria mmoja aliyekuwa akisafiri na ndege ya Qatar Airways kutoka Doha kuelekea Manchester, Uingereza alikamatwa na polisi baada ya kutoa taarifa kuwa ndani ya ndege hiyo kuna bomu, hali iliyomfanya rubani kutoa taarifa kwa mamlaka ya usalama wa anga mara moja. 

Baada ya rubani wa ndege hiyo kujulisha mamlaka husika juu ya abiria kusema kuna bomu katika ndege hiyo, ndege za kijeshi za Uingereza ziliruka haraka na kuisindikiza ndege hiyo hadi ilipotua salama katika uwanja wa Manchester.
                                                   Abira huyo akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi. 

Mara baada ya ndege kutua, polisi waliingia ndani na kumkamata abiria huyo mwenye miaka 47 baada ya kujulikana kuwa taarifa alizotoa zilikuwa za uongo na kusababisha hofu kwa abiria 269 na wahudumu wa ndege 13 waliokuwa ndani ya ndege hiyo aina ya Airbus A330-30
Ndege nyingine zilizuiwa kutua kwa muda katika uwanja huo na kuelekezwa katika viwanja vingine kwa muda.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni