Washika bunduki wa London, Arsenal jana wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza, baada ya kuifunga Manchester City kwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Wimbley.
Manchester City ambao ni abingwa watetezi wa kombe la ligi kuu Uingereza, jana walipoteana kabisa uwanjani kutokana na pasi na mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwao toka kwa vijana wa Arsene Wenger ambao walionekana kusakata kandanda la hali ya juu.
Arsenal ambao ni mabingwa wa kombe la FA, walipata mabao yao kupitia kwa Santi Cazorla katika dakika ya 21, bao la pili likawekwa kimiani na Aaron Ramsey katika dakika ya 42 kabla ya Olivier Giroud kufunga bao la tatu katika dakika ya 60 kipindi cha pili.
Aaron Ramsey akijipinda na kuifungia Arsenal bao la pili dhidi ya Manchester City
Mashabiki wa Arsenal wakiruka kwa furaha wakati timu yao ikiendelea kuwaadhibu Man City hapo jana.
Furaha ya ushindi ni kama hivi




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni