.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 5 Agosti 2014

BAADA YA KUFUTIWA UANACHAMA WAKE SIMBA, WAMBURA KUONGEA NA WAANDISHI WA HABARI LEO

                    Michael Wambura akiwaonesha waandishi wa habari katiba ya Tff. 

Siku chache baada ya timu ya soka ya Simba kutangaza kumfutia uanachama Michael Wambura pamoja na wanachama wengine 70 wa timu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi jijini Dar er Salaam, Wambura leo ataongea na waandishi wa vyombo vya habari kuanika kila anachokiamini kimesababisha yeye kufutiwa uanachama wake. 

Michael Wambura ambaye alijitokeza kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi wa klabu hiyo kabla ya kuenguliwa na kamati ya uchaguzi, hali liyosababisha mivutano mikubwa, amesema hii leo ataaweka hadharani kile ananacho kiamini kuwa ndio sababu ya yeye kufutiwa uanachama. 

Maamuzi ya ya kuwafutia uanachama wa klabu hiyo Wambura na wenzake, yalifikiwa juzi jumapili katika mkutano mkuu wa mwaka wa Simba uliofanyika katika bwalo la maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni