Shirika la Amnesty International
limesema Jeshi la Nigeria limefanya mauaji ya kikatili kaskazini
mashariki wakati likipambana na wapiganaji wa kiislam wa Boko Haram.
Shirika hilo limesema kuna
ushahahidi wa picha za kutisha na za kinyama zikiwemo zile
zinazodaiwa kuonyesha wanajeshi wakiwachinja watu waliokamatwa.
Mamlaka za Nigeria zimesema unyama
kama huo hauruhusiwi jeshini na zimeahidi kuchunguza tukio hilo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni