.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 5 Agosti 2014

BEYONCÉ NA JAY Z KUENDELEA NA TAMASHA LAO PARIS LICHA YA NDOA YAO KUYUMBA

Wanamuziki wanandoa Beyoncé na Jay Z, wanapanga kuendelea na tamasha la mwisho la pamoja Jijini Paris nchini Ufaransa ambalo litarekodiwa na HBO maalum mwezi ujao, licha ya uvumi wa kuvurugika kwa mahusiano yao.

Mahusiano ya wanandoa hao nyota yanasemekana yapo katika mgogoro mkubwa kiasi cha wanasheria wa promota wa tamasha lao la Live Nation kuitwa katika mkutano wa kutafuta ufumbuzi wiki iliyopita.

Hata hivyo tamasha hilo litakalofanyika katika Jiji la mapenzi wa Paris litaendelea kama kawaida kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na HBO na tarehe itakuwa Septemba 20, mwaka huu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni