.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 5 Agosti 2014

NI MSHIKE MSHIKE REDD'S MISS KINONDONI 2014


SHINDANO la kumsaka Redd’s Miss Kinondoni, sasa limefikia patamu baada ya mambo yote kukamilika na kinachosubiriwa ni siku tu ya mchuano wenyewe.

Akithibitisha hilo, Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni, Husna Maulid, alisema kila kitu kimekamilika, huku warembo 20 watakaochuana wakiwa katika mazoezi makali.

Husna alisema, shindano hilo litakuwa la kipekee kutokana na mengine yote yaliyowahi kufanyika na ana uhakika mkubwa hata taji la Redd’s Miss Tanzania litatwaliwa na mrembo kutoka Kinondoni.

“Kwa sasa kinachosubiriwa ni siku tu na warembo 20 wapo katika mazoezi makali kwa ajili ya shindano hilo.”

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Escape one uliopo Mikocheni, Dar es Salaam huku kukiwa na burudani kali toka Malaika Band inayoongozwa na Christian Bella na mwanamuziki wa kizazi kipya anaechipukia kwa kasi Young Suma.

Taji la Redd’s Miss Kinondoni kwa sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na aliyekuwa Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred.

Warembo wanaoshiriki shindano hilo wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani,Ubungo na Dar Indian Ocean, huku kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 30,000 viti maalumu na pia watu mia moja watakaoingia wa kwanza watapata bia moja ya Redd’s original bure kabisa.

Alisema tiketi kwaajili ya shindano hilo zinatarajiwa kuanza kuuzwa rasmi jumatano ya juma lijalo sambamba na zawadi mbalimbali toka kwa wadhamini wa shindano hilo

Wadhamini wa shindano hilo ni Redd’s Original, Kitwe General Traders, CXC Africa,Picolo Hotel, Jambo Leo, Clouds FM, Michuzi Media Group, Father Kidevu blog, Glitters Salon, EFM Redio na Habari mseto blog.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni