.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 12 Agosti 2014

FLAVIANA MATATA FOUNDATION NA PSPF WAKABIDHI VIFAA VYA SHULE LINDI


Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin akimkabidhi begi mmoja wa wanafunzi ambaye ni mlemavu wakati wafanyakazi wa PSPF wakishirikiana na Mwanamitindo Flaviana Matata walipokabidhi vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za Msingi Mtua na Chemchem ziliyopo Nachingwea pamoja nashule za msingi Litingi na Mnengulo ziliyopo Lindi.
Mwanamitindo Flaviana Matata akimkabidhi begi mmoja wa wanafunzi katika shule hizo.


Flaviana Matata akiwa ameongozana na Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin pamoja na wafanyakazi wa PSPF katika zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.

              Mwaamitindo Flaviana Matata akiwa amekaa na wanafunzi darasani.

                                 Mwanamitindo Flaviana Matata akisaini kitabu cha wageni.

Mwanamitindo Flaviana Matata pamoja na wafanyakazi wa mfuko wa pensheni wa PSPF wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi.

Mwanamitondo afanyae kazi zake za mitindo nchini Marekani Flaviana Matata, yuko nchini kwa ajili ya kufanya kazi za kijamii kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation katika mradi wa Back to school project /FMFstationary kit ambao unafadhiliwa na mfuko wa penseni PSPF,

Baada ya mwezi January Flaviana kugawa vifaa shule za msingi za jijini, awamu hii ameenda Mtwara na kufanikiwa kugawa vifaa katika shule za Msingi Mtua na Chemchem ziliyopo Nachingwea pamoja na shule za msingi Litingi na Mnengulo ziliyopo Lindi.

Bado wanaendelea kugawa vifaa hivyo kwa shule za msingi mikoa mingine. 

“hadi sasa tumeshagawa vifaa kwa watoto 700 na bado kuna kits 800 vitasambazwa Tunduma ,Tunduru na Monduli”

Flaviana alitoa shukran kwa PSPF kwa kudhamini huu mradi na akasisitiza makampuni na mashirika kujaribu kuwezesha elimu kama hali halisi inavyoonekana kwenye picha hadi leo kuna wanafunzi wanasoma chini na mti, na walio madarasani,madarasa ni mabovu na hayana madawati.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni