Rais wa Irak akimpongeza Waziri Mkuu Mpya Abdi
Rais Barack Obama wa Marekani
amesema kuteuliwa kwa Bw. Haider al-Abadi kuwa Waziri Mkuu wa Irak ni
hatua muhimu kwa mustakabali wa nchi hiyo.
Obama amesema anatambua kuwa Irak
imekuwa ikipitia katika kipindi kigumu, na kuwasihi viongozi wa
kisiasa kufanya kazi pamoja.
Mapema jana Rais wa Irak, amemtaka
Bw. Abdi kuunda serikali mpya, na kumuacha nje Waziri Mkuu Nouri
Maliki ambaye amenukuliwa akisema uteuzi wa waziri mkuu mpya ni
ukiukaji katiba ya nchi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni