.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 22 Agosti 2014

HAPATOSHI KESHO UWANJA WA TAIFA, REAL MADRID MAGWIJI WAAHIDI KANDANDA LA UHAKIKA DHIDI YA TANZANIA ELEVEN


Mratibu wa Ziara ya Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Real Madrid,Ssebo (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mechi ya kirafiki kati ya Tanzania Eleven na Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Real Madrid kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kesho.Mpaka sasa ni wachezaji watatu tu ndio waliowasili nchini huku wengine kadhaa wakitegemewa kuwasili mchana wa leo.Wachezahi hao ambao wapo nchini hivi sasa ni Luis Figo (wa tatu kulia),Christian Karembeu (kulia) na Beki Fernando Sanz Duran (wa pili kushoto).wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TSN,Farough Baghoza na Kocha wa Timu ya Tanzania Eleven,Jamhuri Kihwelo "Julio"

Kocha wa Timu ya Tanzania Eleven,Jamhuri Kihwelo "Julio" (katikati) akizungumzia namna Timu yake ilivyojiandaa kuwakabili Wakali hao wa soka Duniani wakati wa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye Hoteli ya SouthernSun jijini Dar es Salaam.Kulia ni Luis Figo na kushoto ni Fernando Sanz Duran ambao ni wachezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

Mchezaji Fernando Sanz Duran (kati) nae akitoa maneno yake kuhusu mchezo huo.

                                                            Mwanasoka Christian Karembeu akizungumza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni