.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 11 Agosti 2014

IVORY COAST YATANGAZA KUPIGA MARUFUKU NDEGE KUTOKA NCHI ZENYE EBOLA

Nchi ya Ivory Coast imetangaza kupiga marufuku ndege zote zinazotoka kwenye nchi zinazokabiliwa na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola ikiwa ni hatua za kukabiliana na jitihada za kudhibiti ugonjwa huo kuingia nchini humo.

Serikali imesema imekataza ndege za abiria kutoka nchi hizo kuja Ivory Coast hadi hapo itakapotolewa agizo lingine, na pia imezuia shirika la ndege la taifa la Cote d'Ivoire kwenda katika nchi hizo.

Taarifa hiyo haikutaja nchi hizo lakini takwimu zinaonyesha watu 1000 wamekufa kwa kuugua ugonjwa wa Ebola katika nchi za Liberia, Sierre Leone, Guinea pamoja na Nigeria.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni